Jumanne, 7 Novemba 2017






Mkuu Mpya wa Mkoa wa Manyara Mh. Alexander P. Mnyeti akiwasalimia wakuu wa idara na vitengo wa Sekretariat ya Mkoa, wakuu wa taasisi na watumishi mbalimbali alipowasili kwa mara ya Kwanza kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.












Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mh. Dr. Joel Nkaya Bendera akimpokea na kumkaribisha Mkuu Mpya wa Mkoa wa Manyara Mh. Alexander Pastory Mnyeti aliporipoti kwa mara ya kwanza katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kwa majengo ya Idara za Utawala na Wagonjwa wa Nje (Out Patients).


Muonekano wa Jengo hilo upande wa Mbele 

Muonekano wa Jengo hilo upande wa Nyuma
Ujenzi wa Mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara ikiwa kwenye hatua ya upauji, Mafundi wakiendelea na shughuli zao kama kawaida kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya muda na kwa kiwango kinachotakiwa chini ya Usimamizi wa Mkandarasi wa Majengo Ndugu. Domician Kirina (tarehe 7 Novemba, 2017).

Jumanne, 12 Septemba 2017


Afisa Elimu Mkoa wa Manyara Bwana Anord Msuya katika kikao cha Maafisa Elimu Sekondari akisisitiza Kuhusu usimamizi wa katika utoaji wa Elimu, kuweka mpango mkakati wa Michezo, maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2018 na maandalizi ya mitihani ya Kitaifa katika mazingira ya ufanyikaji.




Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt Joel Bendera akifungua kikao kazi kwa ajili ya kujali mwenendo wa utoaji taaluma katika Mkoa na kujumuisha Wakuu wa Shule za Sekondari zote katika Mkoa na Maafisa Elimu wa Halmashauri zote.




Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt.Joel Bendera, akizindua zoezi la usajili, utambuzi na upigaji chapa wa mifugo, uliofanyika  kijiji cha Hayloto kata ya Nambis  katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu.




Mkuu  wa Mkoa wa Manyara Dkt Joel N. Bendera akiongea na wanafunzi wa Shule  ya Sekondari  Bishop Nicodemus Hhando iliyopo Kata ya Masqaroda Wilaya ya Mbulu Mara alipotembelea katika Shule hiyo ambapo yatafanyika makabidhiano ya Mwenge wa uhuru Kati ya Mbulu  Mji na Mbulu  vijijini.


Ijumaa, 21 Julai 2017

CHANGAMOTO ZA AMCOS ZAWEKEWA MIKAKATI.




Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Eliakim C. Maswi ameongoza kikao cha Chama Kikuu cha Ushirika cha Rift Valley Cooperation Union (RIVACU) na vyama vya msingi vya Ushirika Mkoa wa Manyara na  kujumuisha Vyama vya msingi vya Ushirika (AMCOS) vya Wilaya za Babati, Mbulu, Hanang, Simanjiro na  Kiteto kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara na kuwataka wanaushirika kujikita katika Maendeleo ili kujikwamua kiuchumi.



HATIMAYE BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU LAFUNGULIWA


Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel   N. Bendera akishirikiana na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira wameongoza kikao cha ujirani mwema cha kujadili hatua waliyofikia kulinda Mazingira na viumbe hai hasa samaki katika Bwawa la Nyumba ya Mungu lililofungwa mwezi  Mei 2016 ili kuzuia uvuvi haramu na kuruhusu samaki kuzaliana katika Bwawa hilo.
Aidha, baada ya Kikao hicho kilichofanyika Mkoani Kilimanjaro katika ukumbi wa Mikutano wa Wilaya ya Mwanga, ujulikanao kama Teachers  Learning Centre na kujumuisha Kamati za Ulinzi na Usalama za pande zote mbili, wataalamu mbalimbali na baadhi ya wajumbe kutoka Wilaya ya Simanjiro na mwanga,Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa walikwenda kuongea na wananchi wa kijiji cha nyumba ya Mungu kata ya Ngorika  Wilaya ya Simanjiro ambapo Mheshimiwa Dkt.Bendera alifungua rasmi Bwawa hilo na kuwataka wananchi wa Kijiji hicho kuzingatia maagizo yote ya matumizi ya Bwawa hilo.
Mheshimiwa Dkt.Bendera amesisitiza kuwa kutokana na makubaliano ya kikao cha awali kabla ya Mkutano na wananchi Bwawa hilo litakuwa likifungwa tarehe moja Januari kila mwaka hadi tarehe 30.6 kila mwaka ili kuruhusu samaki kuzaliana.


Maagizo ya Wakuu wa Mikoa ya Kilimanjaro na Manyara kuhusu Bwawa la Nyumba ya Mungu.



Maagizo ya Waheshimiwa wakuu wa Mikoa ya Manyara na Kilimanjaro kwa Halmashauri za Moshi, Mwanga na Simanjiro katika kusimamia utaratibu wa Bwawa la Nyumba ya Mungu ili shughuli za uvuvi ziwe endelevu na zenye tija.
  •  Uundaji wa kamati za forodha BMU (Beach Management Unit) katika kila forodha/Mialo zinazotambulika na kupewa mafunzo.
  • Wavuvi wote lazima wazingatie taratibu za uvuvi zilizowekwa na vikundi vyao vya BMU katika mwalo/forodha husika.
  • Ni lazima vyombo vyote vya uvuvi (Ngalawa, Mitumbwi nk.) kusajiliwa sambamba na ukaguzi wa zana zote za uvuvi ufanyike.
  • Utoaji wa leseni mbalimbali za uvuvi (vyombo vya uvuvi, leseni za uvuvi na leseni ya biashara ya uvuvi) zitatolewa kwa wale ambao wamekidhi viwango vya kupewa lesseni hizo.
  • Vyombo vyote vya uvuvi (Ngalawa Mitubwi nk.) lazima viegeshwe kwenye forodha husika baada ya shughuli za uvuvi na chombo ambacho kitakutwa nje ya forodha husika kitachukuliwa hatua kali.
  • Wavuvi wote watashusha samaki katika mialo/forodha zinazotambulika rasmi atakayekiuka agizo hili atachukuliwa sheria ikiwa ni pamoja na kutaifishiwa samaki.
  • Wavuvi wote wavue samaki wenye ukubwa kuanzia nyanda tatu na kuendelea kama sheria na taratibu za uvuvi zinavyoelekeza.
  • Mtu yeyote haruhusiwi kumiliki, kutumia au kumwachia mtu mwingine kutumia Kokoro,Chandarua, Katuli, Kimia, kokoro ndogo kwa madhumuni ya uvuvi.
  • Samaki wabichi watasafirishwa ndani ya magari maalumu box board yenye barafu yaliyoandikwa maneno SAMAKI TU/FISH ONLY.
  • Ni marufuku kuchanganya mazao ya samaki pamoja na abiria au mizigo mingine yeyote.
  • Kukata ushuru wa samaki katika sehemu husika.
  • BMU na serikali za vijiji zitawajibika kuthibiti uvuvi haramu katika maeneo yao na pale watakaposhidwa kutekeleza agizo hili Afisa Mtendaji wa kijiji mwenyekiti wa kijiji na mwenyekiti wa kitongoji husika hatua kali za kisheria zitachukiliwa dhidi yao.
  • Hairuhusiwi mtu kumiliki sehemu yeyote ya maji (WERA) na ikibainika hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kuzuiliwa kujihusisha na shughuli za uvuvi pamoja na kifungo cha miezi sita au faini isiopungua milioni moja.
  • Wachuuzi wote na wavuvi watawajibika kulipa ushuru wa samaki. Mchuuzi ambaye atakwepa kulipa ushuru huo pindi akibainika na kukamatwa hatua kali zitachukuliwa ikiwa pamoja na chombo cha usafiri kupigwa faini na pia samaki wake watataifishwa.
  • Wakurugenzi wapeleke nakala ya sheria za uvuvi katika kila ofisi ya Mtendaji wa Kijiji kinachohusika na maeneo ya uvuvi ili kuwaelimisha wananchi.


Ijumaa, 31 Machi 2017

WANANCHI WA KIJIJI CHA SHAURIMOYO WAMALIZA MGOGORO NA MWEKEZAJI


Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel N. Bendera amekabidhiwa hati ya shamba lenye ukubwa wa Ekari 1098 lililokuwa likigombewa na wananchi mali ya mwekezaji Bwana PARU Parvinder Nyotta mwenye Kampuni ya Republic Body Builders LTD wa Kijiji cha Shaurimoyo kwa ajili ya kuwagawia wananchi ili kumaliza mgogoro uliodumu kwa zaidi ya mikaka kumi.

WALIMU HANANG WAKUTANA NA MKUU WA MKOA KUBORESHA ELIMU.


Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel N. Bendera akiongea na Walimu wa Shule ya Sekondari na Msingi wa Wilaya ya Hanang' kwa ajili ya kupeana mikakati ya kuboresha ufundishaji katika shule zao.

WATUMISHI WA UMMA MKOA WA MANYARA WAPATA VITAMBULISHO VYA URAIA




Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel N. Bendera amefanya uzinduzi ofisini kwake  wa kugawa Vitambulisho vya Uraia kwa watumishi wa UMMA Mkoa wa Manyara baada ya Mamlaka ya vitambulisho (NIDA) kukamilisha usajili na uhakiki. 


Alhamisi, 30 Machi 2017

ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MAJALIWA (Mb) MKOA WA MANYARA





















Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) akiwasili Mkoa wa Manyara na kupokelewa na Katibu Tawala Mkoa Eliakim C. Maswi katika ziara yake ya kikazi ndani ya Mkoa.

Ziara hiyo ilidumu kwa muda wa Siku tano ambapo alitembelea Wilaya zote za Mkoa wa Manyara ambazo ni Halmashauri za Simanjiro, Kiteto,  Mbulu, Hanang' na Babati.

Ona Ziara hiyo hapa