Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel N. Bendera amekabidhiwa hati ya shamba lenye ukubwa wa
Ekari 1098 lililokuwa likigombewa na wananchi mali ya mwekezaji Bwana PARU
Parvinder Nyotta mwenye Kampuni ya Republic Body Builders LTD wa Kijiji cha
Shaurimoyo kwa ajili ya kuwagawia wananchi ili kumaliza mgogoro uliodumu kwa
zaidi ya mikaka kumi.
Ijumaa, 31 Machi 2017
WALIMU HANANG WAKUTANA NA MKUU WA MKOA KUBORESHA ELIMU.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel N. Bendera akiongea na Walimu wa Shule ya Sekondari na
Msingi wa Wilaya ya Hanang' kwa ajili ya kupeana mikakati ya kuboresha
ufundishaji katika shule zao.
WATUMISHI WA UMMA MKOA WA MANYARA WAPATA VITAMBULISHO VYA URAIA
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel N. Bendera amefanya uzinduzi ofisini kwake wa kugawa Vitambulisho vya Uraia kwa watumishi
wa UMMA Mkoa wa Manyara baada ya Mamlaka ya vitambulisho (NIDA) kukamilisha
usajili na uhakiki.
Alhamisi, 30 Machi 2017
ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MAJALIWA (Mb) MKOA WA MANYARA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) akiwasili Mkoa wa Manyara na kupokelewa na Katibu Tawala Mkoa Eliakim C. Maswi katika ziara yake ya kikazi ndani ya Mkoa.
Ziara hiyo ilidumu kwa muda wa Siku tano ambapo alitembelea Wilaya zote za Mkoa wa Manyara ambazo ni Halmashauri za Simanjiro, Kiteto, Mbulu, Hanang' na Babati.